Methali Zote za Kiswahili (A-Z) - Mhariri (2024)

Methali za Kiswahili

Hapa chini tumekupa methali za Kiswahili zaidi ya 400. Tumezipanga kulingana na herufi:

Methali zinazoanza na herufi A

  • Ada ya mja hunena muungwana ni kitendo.
  • Ada ya mja hunena muungwana ni vitendo.
  • Adhabu ya kaburi aijuaye maiti.
  • Adhabu ya kaburi, aijuaye maiti.
  • Adui wa mtu ni mtu, adui mpende, adui aangukapo mnyanyue.
  • Afadhali ya Musa kuliko ya Firauni.
  • Afya ni bora kuliko mali.
  • Ahadi ni deni.
  • Aibu ya maiti aijuaye mwosha.
  • Aisifuye mvua imemnyea.
  • Alisifuye jua limemwangaza.
  • Ajali haina kinga.
  • Aji*zi ni nyumba ya njaa.
  • Akiba halozi, akiba si mbi ijapokuwa ya kumbi, siku ya kivumbi hutiwa motoni.
  • Akili ni mali, akili nyingi huondoa maarifa.
  • Akili ni nywele kila mtu ana zake.
  • Akili nyingi huondoa maarifa.
  • Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
  • Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.
  • Aliye juu mngoje chini.
  • Aliye kando haangukiwi na mti.
  • Aliyekula kitovu chako hatakuachia utumbo.
  • Aliyekunyima kunde/mbaazi amekupungunguzia mashuzi.
  • Aliyekunyoa shungi kakupunguzia kuchana.
  • Aliyetota hajui kutota.
  • Aliyeumawa na nyoka akiona unyasi hush*tuka.
  • Amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga.
  • Amnyimaye punda adesi ampunguzia mashuzi.
  • Anayemwamini Mungu si mtovu.
  • Angalipaa juu kipungu kamwe hafiki mbinguni.
  • Angurumapo Simba, mcheza nani?
  • Asio mali, hasidi wa mwenye mali.
  • Asiye na bahati habahatiki.
  • Asiye na mwana aeleke jiwe.
  • Asiyejua utu si mtu.
  • Asiyekubali kushindwa si mshindani.
  • Asiyesafiri husifu upishi wa mama yake tu.
  • Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
  • Atangaye na jua hujua.
  • Avumaye baharini papa kumbe wengine wapo.
  • Awali ni awali hakuna awali mbovu.

Methali zinazoanza na herufi B

  • Baada ya dhiki faraja.
  • Baada ya dhiki faraja.
  • Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.
  • Balaa hukutia mtu wako.
  • Bandu bandu humaliza gogo.
  • Bandubandu humala gogo.
  • Baniani mbaya kiatu chake dawa.
  • Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
  • Bao nene si chuma chembamba.
  • Barua ya moyo husomwa juu ya panda la uso.
  • Bendera hufuata upepo.
  • Bilashi, bilashi, katu haitoshi.
  • Binadamu ni kama kilihafu hakosi uchafu.
  • Bura yangu sibadili kwa rehani.
  • Bura yangu sibadili kwa rehani.

Methali zinazoanza na herufi C

  • Chanda chema huvikwa pete.
  • Chelewa chelewa, utakuta mwana si wako.
  • Chombo kilichopikiwa samaki hakiachi kunuka vumba.
  • Chovya chovya humaliza buyu la asali.
  • Chungu kidogo huchemka upesi.
  • Chururu si ndondondo.

Methali zinazoanza na herufi D

  • Dalili ya mvua ni mawingu.
  • Damu ni nzito kuliko maji.
  • Dau la mnyonge haliendi joshi likienda joshi ni matakwa ya Mungu.
  • Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda Mungu kapenda.
  • Dawa ya deni kulipa.
  • Dawa ya jipu kulipasua.
  • Dawa ya moto ni moto.
  • Debe shinda haliachi kutika.
  • Debe tupu haliachi kuvuma.
  • Domo kaya samli kwa mwenye ngombe.
  • Dondandugu halina dawa.
  • Dua la kuku halimpati mwewe.
  • Dunia hadaa ulimwengu shujaa.

Methali zinazoanza na herufi E

  • Eda ni ada yenye faida.

Methali zinazoanza na herufi F

  • Fadhila mpe mama na Mola atakubariki.
  • Fadhila za punda mashuzi.
  • Fadhili ukitenda usingoje shukrani.
  • Fahari isiyo na ari haina heri.
  • Fimbo ya mbali haiuwi nyoka.
  • Fumbo mfumbie mjinga mwerevu huling’amua.
  • Fumbo mfumbie mjinga, mwerevu ataling’amua.
  • Funika kombe mwanaharamu apite.

Methali zinazoanza na herufi G

  • Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.
  • Ghururi na binadamu hawaachani.
  • Ghushi dhahabu na shaba dhambi na dhawabu havighushiki.

Methali zinazoanza na herufi H

  • Haba na haba hujaza kibaba.
  • Hadhari kabla ya hatari.
  • Hakuna bamvua lisilo usubi.
  • Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
  • Hakuna masika yasiyo na mbu.
  • Hakuna masika yasiyokuwa na mbu.
  • Hakuna ziada mbovu.
  • Hamadi kibindo ni silaha iliyo mkononi.
  • Hapana maji yasiyo na mawimbi.
  • Haraka haraka haina baraka.
  • Hasira hasara.
  • Hasira ya mkizi furahaya mvuvi.
  • Hatua moja hufupisha safari.
  • Heri kujikwaa kidole kuliko ulimi.
  • Heri mchawi kuliko mtu fitina.
  • Heri nusu shari kuliko shari kamili.
  • Hewala! si utumwa.
  • Hindi ndiko kwenye nguo na wendao uchi wako.
  • Huenda umaskini ukakaribia ukafiri.
  • Hukutia mtu wako.

Methali zinazoanza na herufi I

  • Ibilisi wa mtu ni mtu.
  • Ingiwa na shake.
  • Inuka twende ni kwa waaganao.
  • Ivushayo ni mbovu.

Methali zinazoanza na herufi J

  • Jambo la ukucha halichukuliwi shoka.
  • Jaribu huleta fanaka.
  • Jawabu la kesho andaa leo.
  • Jawabu wakatiwe na wakatiwe si zani.
  • Jimbi wa shamba hawiki mjini.
  • Jino likingoka ukubwani halimei tena.
  • Jogoo likiwika lisiwikae kutakucha.
  • Jogoo wa shamba hawiki mjini.

Methali zinazoanza na herufi K

  • Kafiri akufaaye si Islamu asiyekufaa.
  • Kamba hukatikia pabovu.
  • Katakata pua uunge wajihi.
  • Katiti ni tamu kingi kina kiembeza.
  • Kazi mbi si mchezo mwema.
  • Kenda fumbata si kumi nenda uje kesho.
  • Kichwa cha kuku hakihimili kilemba.
  • Kidole kimoja hakivunji chawa.
  • Kifo cha wengi harusi.
  • Kila mtoto na koja lake.
  • Kila mwacha samboye, huenda ali mwanamaji.
  • Kila mwamba ngoma,huvutia kwake.
  • Kila mwamba ngoma, ngozi huivuta kwake.
  • Kila ndege huruka kwa ubawa wake.
  • Kilichoingia mjini si haramu.
  • Kilimia kikizama kwa jua huzuka kwa mvua, kikizama kwa mvua huzuka kwa jua.
  • Kilimia kikizama kwa jua, huibukia kwa mvua.
  • Kimya kingi kina mshindo mkuu.
  • Kinyozi hajinyoi akinyoa kujikata.
  • Kinywa ni jumba la maneno.
  • Kipya kinyemi ingawa kidonda.
  • Kisebusebu na kiroho ki papo.
  • Kitanda usicholala huwajui kunguni wake.
  • Kitegwacho kukitega kwataka ubongo.
  • Kivuli cha mgude husaidia walio mbali.
  • Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
  • Kukopa harusi kulipa matanga.
  • Kuku havunji yai lake.
  • Kuku mgeni zawadi za kunguru.
  • Kula kutamu kulima mavune.
  • Kula ni vyepesi lakini kulima ngo.
  • Kula uhondo kwataka matendo.
  • Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
  • Kunguru mwoga hukimbiza bawa lake.
  • Kutoa ni moyo si utajiri.
  • Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
  • Kuvua si kazi kazi ni magawioni.
  • Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi.
  • Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
  • Kuzima kwa koleo si mwisho wa uhunzi.
  • Kwa mwari kwaliwa na kwa kungwi nako huliwa.
  • Kwa mwendawazimu kumeingia mlevi.
  • Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
  • Kwea iliyo uchungu si uongo ulio mtamu.
  • Kwendako mwinyi hurudi mwinyi.
  • Kwenye udongo hukosi mfinyanzi.

Methali zinazoanza na herufi L

La kuvunda halina ubani.

La mgambo likilia kuna jambo.

Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo.

Lila na fila havitangamani.

Lililompata peku na ungo litampata.

Linalopita hupishwa.

Methali zinazoanza na herufi M

  • Mafiga mawili hayainjiki chungu.
  • Mafuu hapatilizwi.
  • Maisha ni bahati ifumbate.
  • Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga.
  • Maji mafu mvuvi kafu.
  • Maji ya nazi hutafuta mvungulio.
  • Maji yakimwagika hayazoleki.
  • Majuto ni mjukuu huja baada ya kitendo.
  • Makuukuu ya mwewe si mapya ya kengewa.
  • Mali bila daftari hupotea bila habari.
  • Mali ilivunja nguu milima ikalala.
  • Mali ya bahili huliwa na mchwa.
  • Mama mkwe hafungui mdomo.
  • Mambo kangaja huenda yakaja.
  • Mashua ya maskini huzama mtoni.
  • Maskini hana kinyongo.
  • Maskini hana rafiki.
  • Maskini haokoti, akiokota huambiwa keba.
  • Mavi usiyoyala wayawingiani kuku?
  • Mavi ya kale hayanuki.
  • Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
  • Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
  • Mbwa wa msasi mkali ni wakali pia.
  • Mcha Mungu si mtovu.
  • Mchagua jembe si mkulima.
  • Mchakacho ujao haulengwi na jiwe.
  • Mchama ago hanyeli huenda akauya papo.
  • Mchawi akifichua mirimo ya wachawi huuawa.
  • Mchele mmoja mapishi mbalimbali.
  • Mchelea bahari si msafiri.
  • Mchelea mwana kulia hulia yeye.
  • Mcheza hawi kiwete ngoma yataka matao.
  • Mchimba kisima huingia mwenyewe.
  • Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
  • Mchovya asali hachovyi mara moja.
  • Mchovya asali hachovyi mara moja.
  • Mdomo siri ya gunda.
  • Meno ya mbwa hayaumani.
  • Mfa maji haachi kutapatatapa.
  • Mfa maji haishi kutapatapa.
  • Mfichauchi hazai.
  • Mfinyanzi hulia gaeni.
  • Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
  • Mgaagaa na upwa, hali wali mkavu.
  • Mganga hajigangi.
  • Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
  • Mgeni njoo mwenyeji apone.
  • Mgomba haushindwi na mkunguwe.
  • Mgonjwa haulizwi dawa.
  • Miye nyumba ya udongo sihimili vishindo.
  • Mkaidi hafaidi hadi siku ya Iddi.
  • Mkamia maji hayanywi.
  • Mkata hana kinyongo.
  • Mkate mkavu wa nyumbani ni bora kuliko nyama ya shuwa ya pengine.
  • Mke ni nguo mgomba ni kupalilia.
  • Mkokoto wa jembe si bure yao.
  • Mkono mtupu haulambwi.
  • Mkono mtupu haurambwi.
  • Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu.
  • Mkuki kwa nguruwe mtamu kwa mwanadamu mchungu.
  • Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
  • Mkwamba hauzai mzabibu.
  • Mkware hajiingilii mwenyewe.
  • Mla mbuzi hulipa ngombe.
  • Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
  • Mlimbua nchi ni mwananchi mwenyewe.
  • Mnyamaa kadumbu.
  • Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
  • Mnyonge hana haki mpaka mwenye nguvu apende.
  • Minyonyore haunuki hupendeza mauaye.
  • Moja shika si kumi nenda rudi.
  • Moja ya mkononi yashida mia ya mbali.
  • Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
  • Mpenzi hana kinyongo.
  • Mpiga ngumi ukuta huumia mkonowe.
  • Mrina haogopi nyuki.
  • Msafiri kafiri.
  • Mshale usio na unyoya hauendi mbali.
  • Mshika mawili moja humponyoka.
  • Mshika mbili moja humponyoka.
  • Mshonaji hachagui nguo.
  • Msi chembe wala uta si muwani.
  • Msitu ni mpya na komba nao.
  • Mstahimilivu hula mbivu.
  • Mtafitafi hula samaki, mtulivu hula nyama.
  • Mtaka cha mvungu ni sharti ainame.
  • Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
  • Mtaka yote hukosa yote.
  • Mtambua ndwele ndiye mganga.
  • Mtaratibu humshinda mwenye nguvu.
  • Mtashi hana kinyongo, ajapowaswa hakomi.
  • Mtembezi hula miguu yake.
  • Mteuzi heshi tamaa.
  • Mti upigwao mawe ni wenye matunda.
  • Mtoto akililia wembe mpe.
  • Mtoto musikivu ndiye abarikiwaye.
  • Mtoto wa nyoka ni nyoka.
  • Muamidi cha ndugu, hufa masikini.
  • Mume ni kazi, mke ni nguo.
  • Mume wa mama ni baba.
  • Mvi usiopambwa vyema huyua.
  • Mvumilivu hula mbivu.
  • Mvuvi ndiye ajuaye pweza alipo.
  • Mwamini Mungu si mtovu.
  • Mwana kidonda, mjukuu kovu.
  • Mwana maji wa kware kufa maji mazoea.
  • Mwana wa mhunzi asiposana huf*ckuta.
  • Mwana wa mhunzi asiposana huvuvia.
  • Mwanamaji hutaraji kufa maji.
  • Mwanzo wa ngoma ni lele.
  • Mwanzo wa mvua ni mawingu.
  • Mwenda juu kipungu hafikii mbinguni.
  • Mwenda pole hajikwai.
  • Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani.
  • Mwenye dada hakosi shemeji.
  • Mwenye kelele hana neno.
  • Mwenye matende hana paja.
  • Mwenye nguvu mpishe.
  • Mwenye tende hana paja.
  • Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
  • Mwizi akishikwa husema kaokota.
  • Mwosha huoshwa.
  • Mwosha huoshwa.
  • Mwosha husitiri maiti.
  • Mzaha mzaha hutumbuka usaha.
  • Mzigo mzito mpe Mnyamwezi aubebe.
  • Mzoea kutwaa, kutoa ni bangu.
  • Mzoea udalali hawezi kazi ya duka.
  • Mzoea vya kunyonga, vya kuchinja hawezi.
  • Mzungu wa kula hafundishwi mwana.

Methali zinazoanza na herufi N

  • Nahodha hodari haogopi mawimbi.
  • Nazi mbovu harabu ya nzima.
  • Ncha ikikosa mshale mzima hukosa.
  • Ndaro haina neno.
  • Ndege mjanja hunaswa kwenye tundu bovu.
  • Ndege wasiofahamu ulimbo hunaswa kumi kumi.
  • Ndoto njema haihadithiwi.
  • Ndovu hashindwi na mkongawe.
  • Ndugu chungu, jirani mkungu.
  • Neno la mbali ni usiku wa giza.
  • Ngalawa isiyo na mirengu haisalimiki.
  • Ngoja ngoja yaumiza matumbo.
  • Ngoja ngoja yaumiza tumbo.
  • Ngozi ivute ili maji.
  • Nguo ya kuazima, haisitiri matako.
  • Nguo ya kuazima haisitiri maungo.
  • Ngombe haelemewi na nunduye.
  • Ngombe mwenye tume ndiye achinjwaye.
  • Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
  • Njaa ya leo ni shibe ya kesho.
  • Njia ya mwongo ni fupi.
  • Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
  • Nyota ya mtu kuzimika.
  • Nyumba ya mgumba haina kilio.
  • Nyumba ya udongo haihimili kishindo.
  • Nzi kufa juu ya kidonda si haramu.

Methali zinazoanza na herufi O

  • Oto la kuku usilaze kicheche.
  • Ondoa dari, uezeke paa.

Methali zinazoanza na herufi P

  • Pahala pa itifaki ikirahi haipiti.
  • Paka akiondoka panya hujitawala.
  • Paka akiondoka panya hujitawala.
  • Paka akiondoka panya hutawala. Paka hakubali kulala chali.
  • Paka mafuta kwa mgongo wa chupa.
  • Palilia mkoche, mnazi wende na nyasi.
  • Pambo la jeneza lamfaani mtu? Panapo udhiapenyeza rupia.
  • Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
  • Pato kuu ni la Mungu apaye wawi na wema.
  • Pema ijapo pema, ukipema sana si pema tena.
  • Pembe za chaki.
  • Penye nia pana njia.
  • Penye uchafu hapakosi nzi.
  • Pilipili usiyoila yakuwashia nini?
  • Pilipili iliyo shambani, yakuwashiani?
  • Pitapita zake hazininyimi usingizi.
  • Polepole ndiyo mwendo.
  • Punda haendi ila kwa mikwaju.

Methali zinazoanza na herufi R

  • Radhi ni bora kuliko mali.
  • Rahisi haihalisi.

Methali zinazoanza na herufi S

  • Samaki mkunje angali mbichi, akishakauka hakunjiki.
  • Samaki mmoja aki huoza wote wameoza.
  • Samaki mmoja aki huoza wote wameoza.
  • Shauku huondoa maarifa.
  • Sheria ni msumeno hukata huku na huku.
  • Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma.
  • Shetani wa mtu ni mtu.
  • Shibe ni mwana malevya na njaa ni mwana malegeza.
  • Shukurani ya punda ni mateke.
  • Sikio la kufa halisikii dawa.
  • Siku njema huonekana asubuhi.
  • Siri ya mtungi aijuaye kata.
  • Siri ya kaburi aijuaye maiti.
  • Sisimizi hawi ngombe.
  • Sitafuga ndwele na waganga tele.
  • Subira yavuta heri.

Methali zinazoanza na herufi T

  • Taa haachi mwiba awe.
  • Tabia ya mtu kupenda mambo ya anasa na starehe.
  • Tikiti baya liko shambani mwako.
  • Titi la mama li tamu, jingine haliishi hamu.
  • Tone na tone huwa mchirizi.
  • Tupa jongoo na mti wake.
  • Turufu huenda kwa mchezaji.

Methali zinazoanza na herufi U

  • Ubaya hatima yake mbaya.
  • Ubishi chanzo cha mateto.
  • Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.
  • Udogo wa kimo una mambo.
  • Uf*ckara hufanya mtu awe na udhalili moyoni.
  • Uhalifu mwenenzi si wa mkazi milele.
  • Uhenga hauambiwi maana.
  • Uislamu umemshinda fisi.
  • Ujana ni moshi ukienda haurudi.
  • Ujanja mwingi mbele giza.
  • Ukiiga tembo kunya utapasuka msamba.
  • Uking’wafua mnofu ukumbuke na kuguguna mfupa.
  • Ukiona ambari na zinduna i papo.
  • Ukiona ambari, zinduna ipapo.
  • Ukiona vyaelea vimeundwa.
  • Ukipenda chongo huita kengeza.
  • Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni.
  • Ukitaja nyoka shika kigongo.
  • Ukitaka kujua utamu wangoma ingia ucheze.
  • Ukitaka kuruka, agana na nyonga.
  • Ukitaka riba sikio ziba.
  • Ukitenda wema usingoje kulipwa.
  • Ukubwa ni jaa.
  • Ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.
  • Ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa.
  • Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.
  • Ulimi hauna mfupa.
  • Ulimwengu ni dhaifu siuoneni sheshe.
  • Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
  • Upeo wa macho si mwisho wa dunia.
  • Ushikwapo shikamana.
  • Usiache mbachao kwa msala upitao.
  • Usidharau dafu embe ni tunda la msimu.
  • Usidharau dafu, embe ni tunda la msimu.
  • Usidharau kiserema chalima kuliko jembe zima.
  • Usicheze na simba ukamtia mkono kinywani.
  • Usigombe na mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
  • Usikate ubeleko mtoto kabla hajazaliwa.
  • Usimlaumu udobi kaniki ni rangi yake.
  • Usimwage mtama kwenye kuku wengi.
  • Usinipake mafuta kwa mgongo wa chupa.
  • Usinivishe kilemba cha ukoka.
  • Usione tanga la nguo ukasahau la myaa.
  • Usipoziba ufa utajenga ukuta.
  • Utajiri ni kivuli.
  • Uuzohali ni nyumba ya njaa.
  • Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
  • Uzuri wa mkakasi ukilowa maji basi.

Methali zinazoanza na herufi V

  • Vita vya panzi, furaha ya kunguru.
  • Vundo la kinyesi ni malazi ya paka/bata.
  • Vunja dari uezeke paa.
  • Methali zinazoanza na herufi W
  • Wajua tamu ya ua, sumu wanipeani?
  • Wanja wa manga si dawa ya chongo.
  • Wapiga mbiu ganjoni utasikiwa na nani?
  • Waraka ni nusu ya kuonana.
  • Wema hauozi.
  • Werevu mwingi mbele giza.

Methali zinazoanza na herufi Y

  • Ya Kaizari mpe Kaizari na ya Mungu mpe Mungu.
  • Ya mgambo ikilia kuna jambo.
  • Ya mkiwa haiiti na ikiita hupapata.
  • Ya mkiwa haiiti, na ikiita hupapa.
  • Yaliyompata peku na ungo yatampata.
  • Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
  • Yaliyopita si uele tugange yajayo.
  • Yuajifanya mawele, kujitia mitini, ili aambiwe naye yumo.

Methali zinazoanza na herufi Z

  • Zana za vita ni silaha.

Soma pia methali 100 na maana zake

Methali Zote za Kiswahili (A-Z) - Mhariri (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Nathanial Hackett

Last Updated:

Views: 6129

Rating: 4.1 / 5 (52 voted)

Reviews: 83% of readers found this page helpful

Author information

Name: Nathanial Hackett

Birthday: 1997-10-09

Address: Apt. 935 264 Abshire Canyon, South Nerissachester, NM 01800

Phone: +9752624861224

Job: Forward Technology Assistant

Hobby: Listening to music, Shopping, Vacation, Baton twirling, Flower arranging, Blacksmithing, Do it yourself

Introduction: My name is Nathanial Hackett, I am a lovely, curious, smiling, lively, thoughtful, courageous, lively person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.